Shirika hili lilianza kama kikundi cha watu wachache sana takribani watu/vijana watano (5) tu mnamo Julai 25, 2017. Lengo la kuanzishwa kikundi hiki ili kuwa ni kutaka kupambana vya kutosha dhidi ya umasikini uliyokithiri katika jamii tunamoishi. Ama kwa hakika tulijikuta tunafanya shughuli za ujaskiriamali kwa maana ya kuandaa karanga na kuziuza, kukaanga mihogo na shughuli zingine ili tuweze kupata fedha ya kutusogeza mbele kwa maana ya kukisajili kikundi chetu.
Mwaka 2018 wanachama wote tuliamua kutafuta uwezekano wa kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kukuza utaalamu wa kile tunaendelea kukifanya kwa jamii. Wakati huu wote tulikuwa kila tunapokutana pamoja tunajadili namna ambavyo tunataweza kusonga mbele ili kutambulika na serikali na viongozi mbalimbali.
Kipindi hiki tukakipa jina kikundi chetu "Co plus group". kwa hiyo tukaendelea kufanya shughuli zetu katika jamii kwa utambulisho wa jina hilo. Kwa kuwa tulipata elimu ya ujasiriamali kutoka kwa Didas Lunyungu (Mjasiriamali kwanza enterprises) tukaweza kutengeneza bidhaa za viwandani kama vile; sabuni za aina zote, dawa za usafi nk; bidhaa za kusindikwa kama vile; karanga za mayai, juisi nk. Lakini kipindi chote hiki tunapata hela ya kututosha kula tu kwa maana ya mtaji kuwa mdogo.
Mnamo tarehe 25/01/ 2019 tulifanikiwa kusajili kikundi katika ngazi ya wilaya. hapa sasa tukaanza kujiamini na kutiwa moyo na wengi ambao walianza kama sisi. Tukawa tunaweza kuendesha semina za ujasiriamali maeneo mbalimbali kwa udhamini wa kampuni ya "MWARECO" ambayo ilikuwa inajishughulisha na uuzaji wa kemikali za kutenganezea sabuni nk. Hivyo wanafunzi wetu waliweza kununua malighafi hizo kwetu na sisi tuliweza kujipatia faida kwa kuuza malighafi na bidhaa tulizo kuwa tunatengeneza na kuziuza.
Mwaka huo huo 2019 tarehe 11 mwezi wa 7 tulifanikiwa kusajili shirika. Hivyo kwa ushauri wa viongozi wa serikali tulishauriwa kubadilisha jina kidogo na kuwa "Community Plus Organization"
kwa maana ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii ambayo yatapelekea kupunguza ukali wa umasikini tulio nao.
Katika mchakato wa kusajili shirika, tuliweza kuwashawishi vijana wengine na kufikia idadi ya vijana wenye nia moja wakike na wa kiume kufikia idadi ya vijana 24. Ambapo wasichana ni 15 na wavulana 09 wa umri kati ya 15 - 45.
Hivyo mpaka sasa tunashirika letu kwa usajili wa wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto. Namba ya usajili ni 00NGO/R/027.
Makao makuu ya shirika ni Mkoa wa Morogoro. Na kwa sasa ofisi zetu zipo wilaya ya Kilombero. Kata ya Mwaya. Kijiji cha Mgudeni. Kitongoji cha Mwamaroba.
Shirika limesajiliwa kwa ngazi ya kitaifa na linamamlaka ya kufanyakazi Tanzania bara isipokuwa \Visiwani (Zanzibar).
Shirika linafanyakazi na kundi la vijana hasa wasichana, na dhima kuu ya shirika ni KUPUNGUZA UMASIKINI ULIOKITHIRI katika jamii kwa kupiga vita; Ujinga, Umasikini na Maradhi. Kwa upande wa pili tunahamasisha utunzwaji wa uoto wa asili kwa maana ya kutunza misitu na vyanzo vya maji.
Mpaka sasa tunajishughulisha na shughuli zetu kwa kushirikiana na serikali za mitaa kwa kibali toka TAMISEMI.
Tungali tunahitaji mawazo, ushauri wa hali na mali ili kuihudumia jamii yetu hii ya Tanzania.
Katika zoezi zimz la kupiga vita umasikini; tumewafundisha vijana wengi kuhusu namna ya kujitengenezea ajira binafsi kwa kuwafundisha kutengeneza sabuni, dawa za usafi na mabatiki Zoezi hili ni endelevu.
Katika kufuta ujinga tunafundisha vijana ujuzi wa Kompyuta na matumizi ya sumu za mkononi kama mtaji wa kujiongezea kipato mahali popote alipo mtumiaji. Lakini pia tunawasaidia kujua kusoma na kuandika watu wazima walio katika VICOBA ili waweze kutunza kumbukumbu zao kwa maandishi na kuwasaidia watoto wao masuala ya shule na kujua maendeleo yao.
Kuhusu kupigana na maradhi tunawashauri wanajamii hasa wajasiriamali wadogo kujiunga na mpango wa bima za afya kwa namna yoyote iliyorahisi.
Shirika pia ni mwanachama wa VICOBA FETA hivyo tunajishughulisha na masuala ya kuvilea vikundi katika mfumo uliorasmi na kwa kufuata vigezo na masharti ya VICOBA Tanzania. Pia tunawajibu wa kuwasogezea uulewa wa fursa mbalimbali zipatikanazo kutoka Baraza la Maendeleo la Taifa na kwingineko ambazo vikundi vingi hasa vya vijijini hawazifahamu.
Kaulimbiu yetu ni "WEZESHA - UWEZESHWE"
Karibu COMMUNITY PLUS ORGANIZATION (COPO)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni